SIMBA WASEMA HAWATARUDIA MAKOSA KWA NDANDA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba SC, wanaingia kambini leo tayari kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu bara dhidi ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara utakaofanyika Jumamosi ijayo katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Simba wanaingia kambini leo kujiandaa na mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kuvuliwa ubingwa wa michuano ya Azam Sports Fedetation Cup, (ASFC) maarufu kombe la FA na timu ya daraja la pili Green Warriors ya Mwenge kwa mabao 4-3 ya mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema hawatakubali kufanya makosa na amesema Ndanda watapata kipigo nyumbani kwao hapo hapo, Simba ipo chini ya kocha msaidizi, Mrundi, Masoud Djuma kufuatia kocha mkuu,Mcameroon Joseph Omog kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya iliyoyapata