RAIS TFF APIGA MARUFUKU MASHINDANO YA NDONDO MCHANGANI
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (Tff) Wallace Karia amepiga marufuku mashindano yote yasiyo rasmi mitaani maarufu kama ndondo hasa yale ya kombe la mbuzi au ng' ombe.
Karia ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba mpya baina ya Tff na kampuni ya Macron ambayo itatengeneza jezi za timu zote za taifa, Rais Karia amewataka watu wanaodhamini mashindano ya ndondo mchangani hasa madiwani, wabunge nk kujitolea udhamini huo kwa timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano hayo ambayo hayatambuliki na Tff.
Kwa kauli hiyo ya kiongozi huyo wa soka nchini, michezo ya ndondo inayochangia kukuza na kuinua viwango vya soka kwa wachezaji wengi hapa nchini sasa haitafanyika tena, tayari baadhi ya wanamichezo wameanza kupingana na kauli hiyo wakimtuhumu Rais huyo wa Tff kwa kudai amekurupuka