YANGA NAO USO KWA USO NA KITIMU CHA DARAJA LA PILI
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, jioni ya leo inatelemka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kucheza na timu ya Daraja la pili ya Reha FC yenye maskani yake Chang' ombe Dar es Salaam mchezo wa raundi ya 64 bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufy kombe la FA.
Yanga ikiwa na furaha ya kurejea kwa mastaa wake waliokuwa majeruhi, itangia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya watani zao Simba ambao juzi waliondolewa katika michuano hiyo na kuvuliwa ubingwa wao na kitimu cha Daraja la pili cha Green Warriors.
Hivyo nao watauchukulia mchezo huo kuwa ni mkubwa kwao kwani watani zao Simba wamemfurusha kocha wao baada ya kipigo hicho, Yanga walivuliwa ubingwa na Mbao FC katika hatua ya robo fainali