Lipuli yanyoosha mikono kwa Asante Kwasi
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Uongozi wa timu ya Lipuli FC "Wanapaluhengo" umemnyooshea mikono mlinzi wake Asante Kwasi raia wa Ghana kujiunga na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC baada ya mvutano mrefu uliodumu karibu majuma mawili kuhusu usajili wake.
Akizungumza leo, mwenyekiti wa Lipuli FC, Ramadhan Mahano amesema umefika mwisho sasa wa kulumbana kuhusu mchezaji Asante Kwasi kwakuwa tayari uongozi wa Simba ulishawafuata na kumuhitaji mchezaji huyo hivyo nao wameona ni bora kuwaachia Simba.
Mahano amesema kuwa Kwasi alikuwa mchezaji halali wa Lipuli waliyemsajili mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Mbao FC ya Mwanza na Simba imekubali kulipa ada ya kumnunua mchezaji huyo ingawa hakuweka wazi ni kiasi gani kitatolewa na Simba.
Mambo Uwanjani inafahamu kuwa Simba itatoa shilingi Milioni 25 kama ada ya usajili kwa mchezaji huyo, Kwasi ataanza kuitumikia Simba kwenye hatua onayofuata ya Ligi Kuu bara na michuano ya kombe la Mapinduzi pamoja na ile ya kimataifa