Azam FC hakuna kuremba, yaifumua Arie C 4-0
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC usiku huu imetinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuifumua bila huruma timu ya Arie C mabao 4-0 uwanja wa Azam Complex , Chamazi.
Mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame wanaonolewa na Mromania, Aristica Cioaba, waliutawala mchezo huo karibu vipindi vyote viwili, hadi mapumziko Azam walikuwa wakiongoza kwa mabao matatu.
Mabao ya Azam yamefungwa na Salmin Hoza dakika ya 17, Agrey Morris dakika ya 34 na Yahya Zayd dakika ya 41 aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Mghana Enock Atta.
Enock Atta naye aliiandikia Azam bao la nne kipindi cha pili dakika ya 53 akiunganisha krosi ya Mzimbabwe Bruce Kangwa, kesho mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC watacheza na Reha FC uwanja wa Uhuru Dar es Salaam