Ndanda wabadili nahodha kisa Simba
Na Mwandishi Wetu. Mtwara
Benchi la ufundi la Ndanda SC limefanya Mabadiliko ya Nahodha wa Klabu ambapo awali Nahodha Mkuu alikuwa Rajabu Zahiri aliyehamia Ruvu shooting Na alikuwa akisaidiwa Na William Lucian Na Jeremia Kisubi.
Kwa Sasa Nahodha Mkuu atakuwa Jacob Masawe akisaidiwa Salum Telela, Jeremia Kisubi na Hemed Khoja.
Haya ni Mabadiliko ya kawaida kufanywa Na Benchi la Ufundi Kwa Majibu wa Kocha Mkuu Malale Hamsini, Ndanda inakabiliwa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya vinara Simba SC, Jumamosi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.