SIMBA MGUU SAWA KUTETEA FA KWA GREEN WORRIORS, KESHO
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kikosi cha Simba jana jioni kiliendelea na mazoezi yake chini ya Kocha Joseph Omog akisaidiana na kocha msaidizi Massoud Djuma.
Akielezea maandalizi ya mchezo maalumu wa ufunguzi wa michuano ya Azam Federetion Cup kocha Omog alisema 'Tunajiandaa vyema kutetea kombe hili, siku ya Ijumaa tutakuwa na mchezo wetu wa kwanza kwenye michuano hii msimu huu dhidi ya Green Warriors na tunaendelea kujiandaa vyema.
Mashabiki waje kwa wingi siku hiyo kwa ajili ya kutupa sapoti ambayo wamekuwa wakitupa kila mahali kikosi chetu kinapokwenda na sisi tunaimani ya kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri'
Kocha Omog amerejea nchini Tarehe 14.12.2017 ambapo alikwenda nchini Cameroon kwenye mapumziko mafupi.