UHURU KENYATA AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI GEORGE WEAH
Rais wa jamhuri ya watu wa Kenya, Uhuru Kenyata amemtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Liberia, George Opong Weah kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa taifa hilo la Afrika magharibi katika uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika mwezi huu.
Weah alimshinda mpinzani wake Joseph Boakai ambaye ni makamu wa rais wa serikali inayomaliza muda wake chini ya rais Helen Johnson Serleaf.
Katika salamu zake, Kenyata ambaye naye alishinda kiti cha urais hivi karibuni, amemsifu Weah kwa ushindi huo na kumtaka aliongoze vema taifa hilo lililowahi kumwaga damu kwa kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Weah anatarajia kuapishwa Januari Mwakani, na pia amewahi kuwa mwanasoka bora wa dunia, akizichezea timu mbalimbali barani Ulaya kama Monaco ya Ufaransa, Ac Milan ya Italia, Man City na Chelsea za England kisha El Jazira ya Uarabuni