YANGA YANOGEWA NA WAKONGOMAN, YAMPA MIAKA MIWILI KAYEMBE

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Mlinzi wa kati toka nchini Congo ( DRC )Finston Festo Kayembe asajiliwa na Yanga SC baada ya majaribio ya muda mrefu! . Yanga imeanza kusuka kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi, ASFC na klabu bingwa Afrika. Kayembe amesaini kandarasi ya miaka miwili.

Kayembe alikuwa na kikosi hicho kwa kipindi kirefu na kiwango chake kimeweza kuwashawishi viongozi wa klabu hiyo pamoja na wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo, kwa usajili huo wa Kayembe ambaye ni beki wa kati, unaondoa uvumi urejeo wa Vincent Bossou raia wa Togo ambaye alitajwa kurejea.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Dissmas Ten, amesema Yanga imemsajili beki huyo ili kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwani wao walikuwa na wachezaji sita.

Kuhusu wachezaji wa ndani, Ten amedai hilo kwa sasa ni jukumu la kocha na mambo yakiwa tayari atawajulisha

Finston Kayembe amesaini miaka miwili Yanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA