Kocha Mbeya City aizimia Yanga, adai ni kiboko
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Kocha mkuu wa Mbeya City, Mrundi, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kwamba mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga SC walistahili kuwashindilia mabao 5-0 kwani wana kikosi bora na hatari msimu huu kuliko timu yoyote inayoshiriki ligi hiyo.
Nsanzurwimo ameyasema hayo alipozungumza na Mambo Uwanjani ambapo amedai kikosi cha Yanga kilicheza vizuri na kuwazidi idara zote wachezaji wake wa Mbeya City.
Lakini kocha huyo aliyechukua mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri, amesema wanajipanga kufanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Singida United ambao amedai nao utakuwa mgumu.
Amedai Yanga iliwazidi mbinu na maarifa na kupelekea kupata ushindi huo mnono, katika mchezo huo Yanga ilipata mabao yake kupitia kwa Obrey Chirwa aliyefunga matatu (Hat trick) na Emmanuel Martin aliyefunga mawili