NDEMLA AFUZU MAJARIBIO SWEDEN

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Said Hamisi Juma (Ndemla) amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden katika klabu ya AFC Eskilistuna ambayo pia anaichezea Mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Ndemla aliondoka majuma mawili yaliyopita kuelekea Sweden na taarifa zilizotolewa na Klabu hiyo aliyofanyia majaribio zinasema amefuzu, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara amefurahishwa na kufuzu huko kwa Ndemla na amesema klabu yao haitasita kumuuza endapo wataafikiana na Eskilistuna.

Manara amesema Simba haina kawaida ya kuwazuia nyota wake wasicheze Ughaibuni hivyo watafanya biashara endapo tu wataafikiana, kesho uongozi wa Simba unakutana kuzungumzia mambo mbalimbali likiwemo hilo ka Ndemla, nyota huyo anatazamiwa kurejea nchini Jumatatu.

Said Ndemla (Kushoto) akiwa Sweden, amefuzu majaribio

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA