Dida mbioni kurejea Simba

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Kuna uwezekano mkubwa klabu ya Simba ikamrejesha aliyekuwa kipa wake wa zamani, Deogratus Munishi "Dida" ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya daraja la pili ya Pretoria University ya nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa ripoti ya kocha wa vinara hao wa Ligi Kuu bara, Mcameroon, Joseph Omog inaonyesha kwamba wanatakiwa wachezaji watatu muhimu ambapo mmoja wa kimataifa anayecheza nafasi ya ushambuliaji na mwingine kipa, Omog pia anamuhitaji kiungo mshambuliaji mzawa ambao mipango ya kuwanasa imeanza.

Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezipata na wala hazina shaka yoyote zinasema kipa Dida ambaye amewahi kuichezea Simba miaka kadhaa iliyopita kabla hajaenda Mtibwa Sugar kisha Azam ambapo baadaye akajiunga na Yanga na kung' ara nayo kisha msimu uliopita kutimkia Afrika Kusini anafaa katika kikosi cha Simba ambao kwa sasa wanahitaji kipa mwingine wa kumpa changamoto Aishi Manula kufuatia Said Mohamed Nduda kuumia.

Hata hivyo alipoulizwa msemaji wa Simba kama kweli kuna taarifa hizo amesema na yeye anasikia tu na wala hakuna ukweli wowote isipokuwa mambo yakiwa tayari watu watatangaziwa kwenye vyombo vya habari kupitia yeye ambaye ndiye msemaji wa klabu

Deo Munishi "Dida" (Katikati) anarejea Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA