IBRAHIM CLASS ATETEA MKANDA WA DUNIA

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Class au King Class, jana mchana ameitoa kimasomaso Tanzania baada ya kufanikiwa kuutetea mkanda wake wa dunia wa Global Boxing Council (GBC) kwakumchapa kwa pointi mshindani wake Cosilia kutoka Afrika Kusini katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Class ambaye alishinda ubingwa huo nchini Ujerumani katika mji wa Berlin kwa kumshinda bondia wa Panama, aliweza kuonyesha kiwango kizuri na kuibuka na ushindi aliopewa bila shaka na majaji, pambano hilo liliudhuriwa na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii, Mhe Dk Harrison Mwakyembe ambaye hata hivyo alimsifu.

Class anakuwa bondia pekee nchini kwa mwaka huu kuitoa kimasomaso Tanzania kutokana na ushindi wake huo ambao unakuwa wa pili kwa ngazi ya mashindano, pambano lake la kwanza lilikuwa Agosti mwaka huu ambalo lilimpa ubingwa wa mkanda huo

Ibrahim Class ametetea mkanda wake jana

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA