Ndanda FC yalazimishwa sare nyumbani
Na Albert Babu. Dar es Salaam
Timu ya Ndanda FC ya Mtwara jioni ya leo imeshindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Njombe Njombe FC ya mkoani Njombe, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hadi timu hizo zinaenda kupumzika zilikuwa hazijafungana yaani 0-0, lakini kipindi cha pili kilionekana kuwa kizuri kwa wageni Njombe Mji ambao wananolewa na Mrage Kabange ambapo walikuwa wakilishambulia lango la Ndanda kama nyuki, Ndanda ilirangulia kupata bao kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa kistadi na William Lucian "Gallas" na Njombe wakasawazisha baada ya kufanya shambulizi kali langoni kwa Ndanda na kuzama kimiani.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumamosi ambapo Yanga SC wataialika Prisons uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mechi nyingine ni Singida United vs Mbeya City, Namfua, Mbao FC vs Mwadui FC, CCM Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar vs Stand United, Kaitaba Stadium.
Nyingine ni Ruvu Shooting vs Majimaji FC, Mabatini Stadium, Mlandizi na Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Simba na Lipuli uwanja wa Uhuru, na siku ya Jumatatu, Azam FC itaikaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi