Prisons yajivunia washambuliaji wake, Yanga itakufa mapemaa
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya
Timu ya soka ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya, imejiweka mguu sawa kuumana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC Jumamosi ijayo katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kocha mkuu wa timu hiyo Mohamed Abdallah amesema hana presha kabisa kuelekea mchezo huo kwani kikosi chake kina washambuliaji wake hatari ambao ni Mohamed Rashid na Eliuta Mpepo ambapo wanaweza kuiua Yanga mapema.
Kocha huyo ametoa ufafanuzi juu ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba katika uwanja wa Sokoine Mbeya ambapo amedai wamefungwa kimchezo lakini Simba ilitegemea bahati zaidi ila watawanyoosha Yanga kwani haiwatishi kabisa na amewataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia soka safi toka kwa vijana wake ambao wanakamata nafasi ya sita.