PROFESA JAY AMWANGUSHA MR TWO SUGU
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Msanii mkongwe na mbunge wa jimbo la Mikumi kupitia Chadema, Joseph Haule "Profesa Jay" leo amemwangusha nguli mwenzake wa hip hop na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi au Mr Two "Sugu" katika shindano la Nani zaidi.
Shindano hilo lililoratibiwa na kituo cha matangazo cha Radio One Stereo chini ya mtayarishaji na mtangazaji mkongwe Abubakar Sadik, Jay ameshinda kwa kura 16 kati ya 2 za Mr Two.
Wawili hao wote ni wabunge wa Jamuhuri ya muungano na pia wamepata kutamba katika medani ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini, akizungumzia pambano hilo, Abubakar Sadiki amesema lilikuwa pambano la aina yake ikizingatiwa wote ni wanasiasa kwa sasa