NGOMA AOTA MBAWA CHALENJI
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Ndoto za mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Donald Ngoma kucheza katika michuano ya kombe la Chalenji sasa imeota mbawa kufuatia nchi yake ya Zimbabwe kujitoa katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba tatu mwaka huu nchini Kenya.
Taarifa kutoka nchini Zimbabwe jana zinasema wameamua kujitoa kwa sababu hali ya usalama nchini Kenya si nzuri hivyo wao wakiwa kama timu mwalikwa wameamua kujitoa.
Chama cha soka Zimbabwe (ZIFA) kimesema kwamba usalama nchini Kenya ni mdogo kufuatia uchaguzi wao ambao umeleta mzozo kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mshindani wake Raila Odinga.
Zimbabwe ilipangwa pamoja na Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini na Burundi hivyo kujitoa kwake kunasababisha timu zibakie nne kwenye kundi lake, Watanzania walitarajia kumtazama Ngoma kupitia michuano hiyo lakini ameota mbawa