Kagera Sugar yaizima Mtibwa, Azam nayo jino kwa jino na Simba
Na Saida Salum. Morogoro
Goli lililofungwa na Christophee Edward "Edo" limetosha kabisa kuipa ushindi wa bao 1-0 Kagera Sugar "Wanamkulukumbi" kutoka Misenyi Bukoba jioni ya leo katika uwanja wa Manungu Complex na kuzima ndoto za Mtibwa Sugar kurejea kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mtibwa Sugar wakicheza nyumbani wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo ili kuzidi kuipa presha Yanga ambao walikuwa sawa kwa pointi lakini wamejikuta wakifia kwa ndugu zao hao wanaotengeneza sukari.
Kipigo hicho kinaifanya Mtibwa Sugar kubaki katika nafasi yao ya nne, Azam FC nayo imeendelea kuifukuzia Simba baada ya kuwalaza wenyeji Njombe Mji bao 1-0 katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, goli lililofungwa na Agrey Morris kwa mkwaju wa penalti, Azam sasa imefikisha pointi 22 sawa na Simba lakini ikizidiwa kwa magoli ya kufunga