Himid Mao awa mchezaji bora wa mwezi, Azam FC
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Kiungo Himid Mao Mkami "Ninja" ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi inayotolewa na klabu yake ya Azam FC, kiungo huyo amewashinda nyota wenzake watatu alioshindanishwa nao kupitia ukurasa wa facebook wa klabu hiyo, Ninja ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars atapewa zawadi yake ya uchezaji bora.
Nahodha wa Azam FC, Himid Mao, anakuwa mchezaji wa tatu msimu huu kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Azam FC (NMB Player Of The Month) baada ya Yakubu Mohammed kufanya hivyo Agosti-Septemba na mshambuliaji Mbaraka Yusuph aliyeibeba Septemba-Oktoba.
Tuzo hiyo inadhaminiwa na Wadhamini wakuu wa Azam FC, Benki ya NMB, ambayo kwa sasa ndio bora kabisa Tanzania ikikuhakikishia usalama wa fedha zako na ikiwa na matawi mengi yaliyosambaa kote hapa nchini