AFANDE SELE AMPONDA MAMA KANUMBA, ADAI SIYO MAMA BORA
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Afande Sele, amesema anashangzwa na kitendo cha Mama Kanumba kushukuru kufungwa kwa Lulu wakati mtoto wake ndiye alikuwa na makosa kwa kuwa na mahusiano na binti mdogo.
Afande Sele amesema mama Kanumba ni mama ambaye hana vigezo vya kuwa mzazi kwani hana uchungu na mtoto wa mwenzake kwenda jela akiwa mdogo, huku ambaye alistahili kuhukumiwa ni mtoto wake Kanumba.
"Mama Kanumba nimeshangaa kusikia anashukuru kwamba Lulu kafungwa, mama ambaye hana uchungu hana sifa ya kuwa mzazi, anashukuru kwamba mtoto mdogo anafungwa kwa ajili ya ubazazi wa mtoto wake, ujinga wa mwanae, upuuzi wa mwanae, mkubwa anambaka mtoto mdogo kama yule”, amesema Afande Sele.
Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama mzazi mwenye mtoto wa kike anatamani hata maiti ya Kanumba ingefukuliwa ichomwe moto ili kuwa fundisho kwa wanaume wengine wenye matendo kama yake.
.