Bocco asema ataendeleza kufunga
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, John Bocco "Adebayor" amesema ataendeleza moto wake wa kufunga kila mchezo kama alivyofanya dhidi ya Tanzania Prisons mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Bocco amesema amepania kuingia katika orodha ya wanaowania kiatu cha dhahabu kwa kufunga kwani uwezo anao na ameshawahi kufanya hivyo, mshambuliaji huyo aliifungia Simba goli pekee la ushindi na kuifanya iendelee kusimama kileleni mwa msimamo wa ligi kwakufikisha pointi 22.
Mshambuliaji huyo kwa sasa amefunga jumla ya magoli mawili na yote amefunga kiustadi mkubwa, Bocco ameahidi kufunga katika michezo inayofuatia ambapo Simba itacheza na Lipuli Jumapili katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi