SIMBA NA LIPULI YARUDISHWA UHURU
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya vinara Simba SC na Lipuli FC ya Iringa uliokuwa ufanyike katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi siku ya Jumapili, sasa umerudishwa katika uwanja wa Uhuru.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema mchezo huo utapigwa uwanja wa Uhuru kwakuwa wamiliki wa uwanja huo serikali haitautumia siku hiyo kwani matumizi ni yanaishia Jumamosi tu ambapo mchezo kati ya Yanga na Prisons utachezewa Azam Complex.
Simba wamepokea kwa mikono miwili mchezo huo kurudishwa uwanja Uhuru wakiamini ndio uwanja wao wa nyumbani na utawapa matokeo mazuri, akizungumza jioni ya leo, Haji Manara ambaye ni msemaji wa vinara hao amesema ni uamuzi mzuri kurudisha mechi hiyo Uhuru