GARDIEL MICHAEL KUREJEA AZAM FC
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam.
Beki wa kushoto wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga SC, Gardiel Michael Mbaga anatazamiwa kurejea katika klabu yake ya Azam FC siku ya Jumamosi pale ambapo atakaposhuka katika uwanja wa Azam Complex kwa mara ya kwanza tangu alipoihama klabu hiyo.
Mbaga kwa sasa anaichezea Yanga SC na Jumamosi mabingwa hao wa bara watautumia uwanja huo kucheza na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara badala ya kuutumia uwanja wa Uhuru ambao umefungwa kupisha shughuri nyingine za kitaifa.
Mlinzi huyo wa kushoto anayemweka benchi Mwinyi Haji Mngwali, atacheza katika uwanja huo ambao alikuwa akiuchezea alipokuwa na kikosi cha Wana lambalamba Azam FC hivyo ni sawa kama anarejea tena katika klabu yake ya zamani lakini kivingine kwa maana atavaa uzi wa kijani na njano unaovaliwa na watoto wa Jangwani