Chalenji Cup, Stars kuanza na waarabu
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, (Cecafa- Chalenge Cup) yamatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 3 hadi 17 mwaka huu katika miji mitatu nchini Kenya.
Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki tayari limetanga makundi mawili ambapo kila kundi lirashirikisha timu tatu huku timu mbili zikiwa mwalikwa, akitangaza makundi hayo ya A na B, katibu mkuu wa Cecafa, Nicolaus Musonye amedai timu zinazoshiriki ni kumi ambapo Kundi A zipo Kenya, Rwanda, Tanzania bara, Zanzibar na Libya.
Kundi B lina timu za Burundi, Ethiopia, Uganda, Sudan Kusini na Zimbabwe, mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Tanzania bara na Libya ambao ni waalikwa, kwa mujibu wa Musonye, michuano ya Chalenji imerejea rasmi ya kukosekana miaka miwili iliyopita na amedai sasa itakuwa ikichezwa kila mwaka.