Yohana Mkomola amfuata Kabwili Yanga
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya chini wa umri wa miaka 23, Yohana Mkomola ambaye pia alikuwemo kwenye kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika Gabon mwaka huu.
Mkomola amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga jana timu ambayo pia anaichezea kinda mwenzake Ramadhan Kabwili.
Mkomola alienda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Tunisia katika klabu ya Esperance, anajiunga na Yanga timu ambayo jana ilimsainisha Mkongoman, Fiston Kayembe kwa mkataba wa miaka miwili.
Hussein Nyika ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili amesema Yanga bado inaendelea kuimarisha kikosi kwakuwa imeandamwa na majeruhi wengi.