YANGA 'INAPENDEZA ZAIDI' YAIUA MBEYA CITY 5-0, CHIRWA ATUPIA MATATU

Na Albert Babu. Dar es Salaam

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imependeza zaidi baada ya kuilaza Mbeya City mabao 5-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mbeya City iliingia uwanjani kwa lengo la kuiuzia Yanga baada ya mchezo wake uliopita kulala nyumbani 1-0 na Simba SC hivyo hawakutaka kupoteza tena leo.

Yanga nao wametoka kulazimishwa sare tasa 0-0 na Singida United hivyo leo ilipania kushinda ikiingia uwanjani bila nyota wake wanne Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Papy Kabamba Tshishimbi na Amissi Tambwe lakini imeweza kunawili.

Magoli ya mabingwa hao watetezi yalifungwa na Obrey Chirwa aliyefunga matatu peke akiondoka na mpira wake na mengine mawili Emmanuel Martin

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA