Duh Maguri kimeeleweka Yanga
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, wanaelekea kukamilisha dili ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na Simba, Elius Maguri ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Dhofar ya Oman aliyojiunga nayo misimu miwili iliyopita.
Uongozi wa Yanga umeweka bayana kumuhitaji Maguri kwakuwa atawasaidia kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani, Maguri ana uwezo mkubwa wa kufunga na amekuwa akifanya hivyo katika timu ya taifa, Taifa Stars.
Katika mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Benin, Maguri aliifungia Tanzania goli la kusawazisha na kufanya matokeo yawe 1-1, Na Yanga wameamua kumnasa Maguri wakitaka ushirikiano wake na akina Ibrahim Ajibu, Obrey Chirwa na Raphael Daudi kwenye safu ya ushambuliaji