KOCHA WA PRISONS AIDHARAU SIMBA NA KUWAAMBIA KIPIGO KIPO PALEPALE
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Prisons, Mohamed Abdallah, ameielezea mechi ya leo dhidi ya Simba na kusema ushindi kwa timu yake upo palepale akikumbushia ushindi wa mabao 2-1 walioupata msimu uliopita dhidi ya Simba.
Leo jioni katika uwanja wa Kumbukumbu ya Edward Moringe Sokoine jijini Mbeya kutapigwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania baina ya Wajelajela na Wekundu wa Msimbazi ambapo wenyeji Prisons wamedai Simba si timu kubwa ila ni timu kongwe hivyo watawahenyesha na ukongwe wao.
Kocha huyo anajiamini kuliko maelezo hasa kutokana na kikosi chake kuwa na pointi 14 huku kikionyesha ushindani wa hali ya juu, Prisons inamtumainia mshambuliaji wake Mohamed Rashid ambaye mpaka sasa amefunga mabao matano