Kill Stars kupaa zao usiku wa leo
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars kinatarajia kusafiri leo usiku kuelekea Kenya tayari kwa kushiriki michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Chalenji, kikosi hicho kilikuwa kikijifua chini ya kocha Amme Ninje na jana kimeongeza nyota wengine watatu ili kukipa makali na ikiwezekana kurejea na kikombe.
Kocha wa kikosi hicho ameamua kuongeza nyota wengine watatu na kufanya jumla ya wachezaji walioteuliwa kujiunga na kikosi hicho kufikia 22, waliojumuhishwa jana ni kipa wa Yanga SC, Ramadhan Kabwili, Aman Kiata wa Nakuru All Stars ya Kenya na mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Yahaya Yazed.
Kill Stars imepamgwa pamoja na wenyeji Kenya, Libya, Zanzibar na Rwanda ambapo michuano hiyo inatazamiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili ijayo na viwanja viwili vimepangwa kutumika