Profesa Jay na Mr Two kupambanishwa kesho

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Wasanii mashuhuri wa Hip Hop waliopata mafanikio makubwa hapa nchini, Joseph Haule "Profesa Jay" na Joseph Mbilinyi "Mr Two" wanatazamiwa kupambanishwa kesho Jumapili katika kituo cha Radio One Stereo kupitia kipindi chake cha Nani Zaidi kinachoanza kusikika kuanzia saa 8 kamili mchana hadi saa 10 jioni.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi hicho Abubakar Sadik "Kwa fujo" amesema hilo ni pambano kubwa na kali ambalo litawasisimua wengi.

Wawili hao kwa sasa wote ni wabunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakichaguliwa katika majimbo yao ya Mikumi (Haule) na Mbeya mjini (Mbilinyi) kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)

Joseph Haule (Kulia) akiwa na Joseph Mbilinyi (Kushoto) wanapambanishwa kesho na Radio One

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA