Azam FC yamnasa Mghana mwingine hatari

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Baada ya kuachana na straika wake Yahaya Mohamed ambaye ni raia wa Ghana, uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unayofuraha kuwajulisha kuwa imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur, akitokea Liberty Professional ya Ghana.

Taarifa kamili zinasema kwamba Mghana huyo amepewa mkataba wa miaka miwili ingawa msemaji wa klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Jaffar Idd Maganga amekataa kuzungumzia usajili huo na kudai kesho ndio wataanika kila kitu.

Azam inaonekana imenogewa na wachezaji wanaotokea Ghana, kwani mbali na kuachana na Mghana, Yahaya Mohamed ambaye ameshindwa kuushawishi uongozi wa timu hiyo lakini ikaamua kumnasa Mghana mwingine na kufanya kikosi hicho kutawaliwa na nyota wa kigeni kutoka Ghana nchi iliyoko ukanda wa Afrika magharibi

Benard Athur (Kushoto) akitambulishwa rasmi kusajiliwa na Azam FC

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA