Simba nao kama Yanga, washikwa na 'Wanapaluhengo'

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC nao kama Yanga, baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare na 'Wanapaluhengo', Lipuli FC ya Iringa ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba walikuwa wa kwanza kujipatia bao la uongozi lililofungwa na kiungo wake mkongwe Mwinyi Kazimoto lakini Lipuli wakasawazisha kupitia Asante Kwasi na kufanya mchezo huo kuamuliwa kwa sare.

Sare hiyo inafanana na ile ya watani wao Yanga ambao jana walilazimishwa na Prisons ya Mbeya ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Simba sasa imefikisha pointi 23 ikiendelea kukaa kileleni ikiwa imecheza mechi 11, kesho Azam FC itakuwa na kazi nyepesi ya kukamata kiti cha uongozi itakapoialika Mtibwa Sugar katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi, Azam ina pointi 22 na ikishinda tu itakaa kileleni

Mwinyi Kazimoto ameinusuru Simba leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA