Lipuli yaweka ngumu kwa Asante Kwasi kwenda Simba
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Uongozi wa timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa, umemzuia kiungo wake Mghana, Asante Kwasi kujiunga na vinara wa Ligi Kuu bara, Simba SC kama ilivyodaiwa hivi karibuni.
Simba iimteka Kwasi kwa masaa manne ili kuteta naye ikitaka kumpa mkataba lakini Lipuli wameshituka na kudai mchezaji huyo haendi kokote na bado ana mkataba wa kuitumikia timu yao.
Asante Kwasi alimtungua kipa wa Simba, Aishi Manula kwa shuti la mbali na kufanya matokeo yawe 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika Jumapili iliyopita uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Simba na Yanga zimenogewa na mchezaji huyo aliyejiunga na Lipuli mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mbao FC ya jijini Mwanza.