Mtangazaji Clouds ampeleka Singano Yanga
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha kituo cha matangazo cha Clouds Fm, Issa Maeda amelitaka benchi la ufundi la mabingwa wa soka nchini, Yanga SC kumsajili kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano Messi ili aweze kuisaidia timu hiyo katika kutetea taji lao pamoja na uwakilishi wa nchi mwakani.
Maeda aliyesema hayo juzi katika kipindi chake cha michezo kinachoanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 usiku, mtangazaji huyo amedai Yanga inahitaji winga mwenye kasi kama ilivyokuwa kwa Simon Msuva ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa Morocco katika klabu ya Difaa El Jadida.
Singano anafaa kuisaidia Yanga hivyo uongozi wa Yanga unapaswa kumtazama kwani kwa sasa winga huyo aliyelelewa na kukuzwa na timu ya Bom Bom ya Kariakoo kisha akajiunga na Simba SC, anaichezea Azam FC lakini amekuwa hapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza