Waziri Mwakyembe azuia Simba kukabidhiwa kwa mwekezaji Jumapili
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe, amesema kwa mujibu wa sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania, hairuhusu klabu yoyote ya michezo inayomilikiwa na wanachama kuuza Hisa kwa asilimia zaidi ya 49.
Mwakyembe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na chombo kimoja cha habari ambapo amefafanua kuwa klabu inayomilikiwa na mtu binafsi ndiyo inaruhusiwa kuuza hisa zaidi ya 49 na kumilikiwa na mwekezaji.
Kwa maana hiyo Mwakyembe amezuia mchakato wa kumkabidhi mwekezaji aliyeshinda zabuni ya kununua Hisa asilimia 50 za klabu ya Simba, ambapo Jumapili ya Desemba 3 itamtambulisha kwa wanachama na kupewa klabu aiendeshe.