Kapuya asema Simba ikizubaa tu, Yanga bingwaa VPL
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Aliyekuwa waziri wa elimu, utamaduni na michezo katika awamu ya tatu ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Profesa Juma Othman Kapuya, ambaye ni mpenzi na mwanachama wa klabu ya Simba, amesema kama timu yake anayoishabikia itazubaa kama ilivyokuwa misimu iliyopita, watani zao Yanga SC watabeba tena ndoo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Kapuya aliyasema hayo juzi Jumapili wakati Simba ilipocheza na Lipuli ya Iringa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba ilitoshana nguvu na Lipuli kwa kufungana bao 1-1 na alipoitazama vema Simba, Kapuya akatikisa kichwa na kutamka Simba ikizubaa tu, Yanga bingwa.
Waziri huyo hivi karibuni alitembelea makao makuu ya klabu ya Yanga na kupokelewa na katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambapo alitembezwa hadi maktaba na kuonyesha makombe mbalimbali iliyotwaa klabu hiyo.
Kapuya alikabidhiwa kombe la Ligi Kuu ya Bara ambalo Yanga imelitwaa mara tatu mfululizo, mdau huyo mkubwa wa soka nchini ambaye amewahi kumiliki bendi ya Akudo, amewasifu Yanga akidai wana umoja na mshikamano ambao umewawezesha kutwaa VPL mara nyingi na katika mazingira magumu