ZFA YAKANUSHA KUANIKA RATIBA YA KOMBE LA MAPINDUZI
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Chama cha soka Zanzibar, (ZFA) imesema hawaitambui kabisa ratiba iliyotolewa jana ya kombe la Mapinduzi ambayo inasema michuano hiyo itaanza Desemba 30 huku timu 10 zikitajwa katika makundi mawili, Katibu mkuu wa ZFA ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati ya mashindano hayo, Sheikh Khamis Abdallah, amesema ile ratiba iliyotolewa jana na kusambazwa mirandaoni ni feki.
Sheikh Abdallah amedai ni kweli michuano hiyo itashirikisha timu 10 na wameialika URA ya Uganda lakini ratiba iliyotangazwa si yao ometengenezwa na watu wachache wanaotaka kuharibu mambo yao, pia katika mashindano hayo timu ya Shaba ya Pemba hawajaialika isipokuwa kwenye ratiba feki imejumuhishwa.
Ratiba hiyo iliyotolewa jana ilisema kuwa kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza rasmi visiwani Zanzibar kuanzia Desemba 30 mwaka huu na kumalizika Januari mwakani, ambapo jumla ya timu 10 zinarajiwa kushiriki huku timu moja ikiwa ni mwalikwa.
Chama cha soka Zanzibar (ZFA) kimezitaja timu za URA ya Uganda ambayo imepangwa kwenye kundi A lenye timu za Simba SC, Azam FC, Jamhuri ya Pemba, Taifa Jang' ombe na URA ya Uganda wakati kundi B lina timu za Yanga SC, JKU, Zimamoto, Mlandege na Shaba ya Pemba.