BOCCO AZIMA NGEBE ZA WAJELAJELA
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Goli lililofungwa kunako dakika ya 85 na mshambuliaji John Rafael Bocco "Adebayor" limetosha kabisa kuipa pointi tatu Simba SC baada ya kuilaza Tanzania Prisons bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Mchezo huo uliomalizika jioni hii ulikuwa mkali na wa kusisimua na kila timu ilijaribu kupeleka mashambulizi langoni kwa mwenzie, mechi hiyo ngumu imefanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Edward Moringe Sokoine jijini Mbeya na Simba kuweza kujizolea pointi sita na sasa ikifikisha pointi 22 ikiwa imeshuka uwanjani mara kumi.
Mchezo wa leo umekumbushia ule wa msimu uliopita uliofanyika katika uwanja huo huo wa Sokoine ambapo vijana wa Prisons waliweza kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Victor Hangaya ambaye kwa sasa amejiunga na Mbeya City