Uganda ipo kamili kwa Chalenji, Okwi atemwa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Moses Basena, ameita kikosi cha wachezaji 24 watakaochujwa hadi kubakia 22 watakaosafiri Jumamosi ijayo kuelekea Nairobi Kenya tayari kwa kushiriki michuano ya kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Desemba 3 mwaka huu.
Katika kikosi kilichotangazwa na Basena ambaye amewahi kuinoa klabu ya Simba ya Tanzania, amemtema kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Emmanuel Okwi anayeichezea Simba lakini akamjumuhisha beki kisiki anayekipiga Simba, Jjuuko Murushid, Okwi amefunga mabao manane huku klabu yake ikiwa kileleni.
Michuano ya chalenji itafanyika mwaka huu baada ya kukosekana kwa muda wa miaka miwili na Uganda ndio mabingwa watetezi, hivyo Basena amekiandaa vema kikosi chake