Ni zamu ya Yanga kukaa kileleni leo

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC jioni ya leo wana nafasi kubwa ya kurejea kileleni endapo wataifunga Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Na kwa bahati nzuri Yanga leo itakuwa imetimia hasa baada ya kurejea kwa mastaa wake Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe ambao walikuwa majeruhi.

Lakini pia kinara wake wa magoli, Obrey Chirwa pamoja na kiungo mshambuliaji mbunifu Ibrahim Ajibu watakuwa chachu ya ushindi katika mchezo huo.

Prisons nao siyo wa kubeza kwani wana washambuliaji wao hatari Mohamed Rashid na Eliuta Mpepo ila wanaweza kutulizwa na Kevin Yondan na Vincent Andrew.

Yanga ina pointi 20 ikiwa imecheza mechi 10 na leo utakuwa mchezo wake wa 11 na kama itashinda itafikisha pointi 23 ambapo zitakuwa nyingi zikiwaacha nyuma Simba na Azam zenye pointi 22 kila moja ila zenyewe zitazidiwa mchezo mmoja.

Simba wao watacheza kesho na Lipuli katika uwanja wa Uhuru wakati Jumatatu Azam FC itachuana na Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Yanga leo wanarejea kileleni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA