KAMUSOKO, TAMBWE WAREJEA MAZOEZINI YANGA, PRISONS MJIPANGE MSIJE KUPIGWA MKONO KAMA NDUGU ZENU

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Nyota wa kigeni wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko na Mrundi, Amissi Joselyin Tambwe leo wameanza mazoezi rasmi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kukosekana kwa kipindi kirefu.

Kamusoko aliumia na kukosa mechi kadhaa za klabu yake na Amssi Tambwe alishindwa kabisa kuitumikia Yanga tangu inaanza msimu mpya naye akiwa na majeraha, lakini nyota hao wawili leo wameungana na wenzao na kurudisha matumaini mapya kwa mabingwa hao ambao Jumamosi ijayo watashuka kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi kucheza na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Yanga iliichabanga Mbeya City mabao 5-0 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam wikiendi iliyopita bila kuwepo mastaa wake hao, hivyo kwa uwepo wao, Prisons inaweza kuchabangwa zaidi ya mabao hayo kama haijagangamala

Thabani Kamusoko (Kushoto) amerejea mazoezini leo, (Kulia) ni kocha George Lwandamina

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA