TP MAZEMBE WABEBA NDOO YA SHIRIKISHO AFRIKA
Timu ya soka ya TP Mazembe ya jamuhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) jana usiku imetawazwa kuwa mabingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika,baada ya kulazimisha sare tasa 0-0 ya ugenini dhidi ya Supersport ya Afrika Kusini katika uwanja wa Lucas Moripe mjini Tshwane.
TP Mazembe wanakuwa mabingwa kufuatia ushindi wake wa mabao 2-1 ilioupata mjini Lubumbashi wiki iliyopita, huo unakuwa ubingwa wa pili mfululizo kwa timu hiyo ambapo pia ni rekodi nyingine kwa kocha wake Pamphile Mihayo ambapo sasa anakuwa kocha wa 10 Mwafrika kubeba taji hilo.
Ubingwa huo wa pili mfululizo kwa TP Mazembe kunarejesha heshima ya timu hiyo inayoonekana kupotea hasa baada ya kuondolewa katika hatua za mwanzoni za Ligi ya Mabingwa barani Afrika