Bossou arejea Yanga kiaina
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Beki wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou ametangaza kurejea Yanga baada ya kuikacha msimu huu akitaka kuongezewa donge nono pamoja na mshahara lakini kwa bahati mbaya aliyekuwa akitoa pesa hizo aliingia matatizoni na Yanga hakuna pesa na kuamua kutimkia kwao.
Lakini baada ya kusikia mambo yameanza kuwa safi na umuhimu wake bado unahitajika akaamua kumtwangia simu kocha mkuu, Mzambia George Lwandamina na kwa bahati nzuri Lwandamina anamuelewa akaamua kuliorodhesha jina lake katika nyota anaowahitaji na tayari viongozi wa Yanga wameweka wazi kuwa beki huyo lazima wamnase ili kuimarisha kikosi chao.
Bossou amewahi kuichezea Yanga kwa misimu miwili na kuiongoza kutwaa ubingwa wa Tanzania bara mara mbili mfululizo, na akaamua kutimka zake baada ya kushindwana na viongozi juu ya kusalia katika kikosi hicho.
Hata hivyo Bossou ameamua kurejea kufuatia mipango yake ya kucheza soka nchini Vietnam kukwama na kuiomba klabu yake ya zamani ya Yanga impe tena nafasi ili aendeleze makamuzi yake