KOMBE LA MAPINDUZI KUANZA DESEMBA 30, SIMBA NA YANGA NDANI
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar
Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza rasmi visiwani Zanzibar kuanzia Desemba 30 mwaka huu na kumalizika Januari mwakani, ambapo jumla ya timu 10 zinarajiwa kushiriki huku timu moja ikiwa ni mwalikwa.
Chama cha soka Zanzibar (ZFA) kimezitaja timu za URA ya Uganda ambayo imepangwa kwenye kundi A lenye timu za Simba SC, Azam FC, Jamhuri ya Pemba, Taifa Jang' ombe na URA ya Uganda wakati kundi B lina timu za Yanga SC, JKU, Zimamoto, Mlandege na Shaba ya Pemba.
Azam FC ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kuifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainali, michuano hiyo kwa sasa imekamata chti katika ukanda huu