Tutaichakaza Prisons- Djuma
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Kocha msaidizi wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Mrundi,Masoud Djuma amesema kikosi chake leo kitachomoza na ushindi dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Masoud Djuma amesema ana kila sababu ya kukiongoza kikosi chake kushinda leo kwakuwa kimeimarika vya kutosha.
Simba ilipotoka kuichapa Mbeya City 1-0 ikaenda Katavu kisha Sumbawanga kujiandaa na mchezo huo hivyo ushindi ni lazima, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kushangilia mwanzo mwisho kwani matokeo ni jambo la kawaida kwao