Chanongo arejea kuipa nguvu Mtibwa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mambo yameanza kuwa mazuri kwa Mtibwa Sugar baada ya kurejea tena uwanjani kwa kiungo mshambuliaji wake Haroun Chanongo kufuatia kupona majeraha yake ya goti yaliyomweka benchi kwa kipindi cha miezi sita.
Chanongo aliyejiunga na wakata miwa hao wa Manungu akitokea Stand United ambayo alijiunga nayo akitokea Simba SC, anaweza kuwa msaada kufuatia kikosi hicho kupoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex, Morogoro.
Meneja wa mchezaji huyo Said Ibrahim amesema kwamba, Chanongo amerejea katika kikosi hicho kuhakikisha anakisaidia ili kuweza kufanya vema katika ligi inayoendelea ambayo mpaka sasa Mtibwa Sugar inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 17 katika mechi kumi ilizocheza