Kilimanjaro Stars yatangaza kikosi cha Chalenji Cup

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars imetangaza kikosi chake ambacho kitashiriki michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati (Cecafa Chalenge Cup) ambayo kwa mwaka huu yatafanyika nchini Kenya kuanzia Desemba 3 hadi 17.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Amme Ninje ametangaza kikosi huku akimtema winga Simon Msuva anayeichezea Difaa El Jadida ya Morocco na kumjumuhisha Danny Lyanga anayeichezea Fanja FC ya Oman.

Akitangaza kikosi hicho jana, Ninje ambaye amewahi kuichezea Stars miaka iliyopita ameita wachezaji 20.

Ambao ni makipa: Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United), mabeki: Boniface Maganga (Mbao FC), Gardiel Michael (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Mohamed Hussein "Tshabalala", (Simba SC) na Kennedy Wilson.

Viungo: Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Tusker, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daudi (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Ajibu (Yanga SC), Abdul Hilal (Sony Sugar, Kenya).

Washambuliaji: Elius Maguri (Huru), Mbaraka Yusuf (Azam FC), Yohana Mkomola (Huru) na Danny Lyanga (Fanja FC ya Oman).

Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A pamoja na ndugu zao Zanzibar , wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya

Kikosi cha Kilimanjaro Stars

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA