DEGE LA TP MAZEMBE LAZUIWA KUTUA DRC
Rais wa jamuhuri wa kidemokrasia ya Congo, (DRC) Joseph Kabila amezuia ndege iliyobeba wachezaji wa TP Mazembe ambao walikuwa wakitokea nchini Afrika Kusini walikotoka kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika.
Kabila ameingiza masuala ya siasa, baada ya kuzuia ndege inayomilikiwa na timu hiyo isitue DRC na badala yake ikatua Ndola, Zambia na baadaye kuchukua usafiri wa basi na kuelekea Lubumbashi.
Kabila amekuwa na uhasama wa kisiasa na mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Katanga na pia aligombea urais wa DRC kisa kilichopelekea ashikiliwe na baadaye kukimbia nchi