Ndanda na Njombe Mji FC kazi ipo kesho Nangwanda Sijaona
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara itaendelea kesho kwa mchezo mmoja ambapo Ndanda FC itawakaribisha Njombe Mji FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi ambapo Yanga wataialika Prisons uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mechi nyingine ni Singida United vs Mbeya City, Namfua, Mbao FC vs Mwadui FC, CCM Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar vs Stand United, Kaitaba Stadium.
mechi nyingine Ruvu Shooting vs Majimaji FC, Mabatini Stadium, Mlandizi na Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Simba na Lipuli uwanja wa Uhuru