Tanzania yazidi kutota FIFA

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Tanzania imeendelea kuporomoka kwenye viwango vya ubora wa kandanda duniani vinavyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), Shirikisho hilo jana lilitangaza viwango vipya ambapo Tanzania imezidi kushuka kutoka nafasi ya 136 hadi ya 142 ikionekana kudondoka kwa nafasi sita zaidi.

Licha ya kulazimisha sare ya ugenini dhidi ya Benin ya kufungana bao 1-1 lakini bado haikuweza kuishawishi FIFA kuipandisha juu Tanzania, katika mchezo huo Tanzania ilicheza vizuri na kuweza kuwabana wenyeji ambao walitangulia kupata bao la kuongoza ambalo lilikuwa la utatanishi.

Goli hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza lakini mwamuzi wa mchezo huo ni kama aliwapa penalti hiyo kwa dhumuni la kuibeba Benin kwani mchezaji wa Benin ndiye aliyeunawa mpira lakini penalti ikaelekezwa langoni kwa Tanzania.

Elius Maguri aliisawazishia Tanzania na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare, katika viwango hivyo, Senegar imekuwa kinara kwa hapa Afrika na Uganda imeonekana kinara katika ukanda wa Afrika mashariki, huku Ujerumani na Brazil ziking' ara kileleni

Tanzania imeshuka tena viwango FIFA

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA